parentingtanzania.family.blog Open in urlscan Pro
192.0.78.31  Public Scan

Submitted URL: https://www.parentingtanzania.family.blog/
Effective URL: https://parentingtanzania.family.blog/
Submission Tags: falconsandbox
Submission: On November 29 via api from US — Scanned from US

Form analysis 3 forms found in the DOM

POST https://subscribe.wordpress.com

<form method="post" action="https://subscribe.wordpress.com" accept-charset="utf-8" style="display: none;">
  <div>
    <input type="email" name="email" placeholder="Enter your email address" class="actnbr-email-field" aria-label="Enter your email address">
  </div>
  <input type="hidden" name="action" value="subscribe">
  <input type="hidden" name="blog_id" value="187583795">
  <input type="hidden" name="source" value="https://parentingtanzania.family.blog/">
  <input type="hidden" name="sub-type" value="actionbar-follow">
  <input type="hidden" id="_wpnonce" name="_wpnonce" value="598a68b44f">
  <div class="actnbr-button-wrap">
    <button type="submit" value="Sign me up"> Sign me up </button>
  </div>
</form>

<form id="jp-carousel-comment-form">
  <label for="jp-carousel-comment-form-comment-field" class="screen-reader-text">Write a Comment...</label>
  <textarea name="comment" class="jp-carousel-comment-form-field jp-carousel-comment-form-textarea" id="jp-carousel-comment-form-comment-field" placeholder="Write a Comment..."></textarea>
  <div id="jp-carousel-comment-form-submit-and-info-wrapper">
    <div id="jp-carousel-comment-form-commenting-as">
      <fieldset>
        <label for="jp-carousel-comment-form-email-field">Email (Required)</label>
        <input type="text" name="email" class="jp-carousel-comment-form-field jp-carousel-comment-form-text-field" id="jp-carousel-comment-form-email-field">
      </fieldset>
      <fieldset>
        <label for="jp-carousel-comment-form-author-field">Name (Required)</label>
        <input type="text" name="author" class="jp-carousel-comment-form-field jp-carousel-comment-form-text-field" id="jp-carousel-comment-form-author-field">
      </fieldset>
      <fieldset>
        <label for="jp-carousel-comment-form-url-field">Website</label>
        <input type="text" name="url" class="jp-carousel-comment-form-field jp-carousel-comment-form-text-field" id="jp-carousel-comment-form-url-field">
      </fieldset>
    </div>
    <input type="submit" name="submit" class="jp-carousel-comment-form-button" id="jp-carousel-comment-form-button-submit" value="Post Comment">
  </div>
</form>

POST

<form method="post">
  <input type="submit" value="Close and accept" class="accept"> Privacy &amp; Cookies: This site uses cookies. By continuing to use this website, you agree to their use. <br> To find out more, including how to control cookies, see here: <a href="https://automattic.com/cookies/" rel="nofollow">
			Cookie Policy		</a>
</form>

Text Content

Skip to content


PARENTINGTANZANIA

Today's Children Tomorrow's Parent

Menu + × expanded collapsed
 * Home
 * About
 * Blog
 * Contact

 * Facebook
 * Twitter
 * Instagram


MALEZI YA MTOTO NA USALAMA SHULENI

Malezi ya mtoto na usalama shuleni husaidia kuleta matokeo chanya kwa mwanafunzi
na mwalimu katika mazingira ya shulen. Shuleni kunakuwa sehemu salama pale
ambapo wanafunzi, walimu na watenda kazi wengine wameekewa mazingira rafiki
yanachangia kujifunza, Afya njema na mahusioano mazuri.

USALAMA SHULENI UNAZINGATIA

Usalama wa mwili

Usalama wa akili

Usalama wa kihisia

Mahusiano na muingiliano mazuri

Mazingira yenye muongoo na kujifunza kwa vitendo

Muunganisho wa shule kwa kujaliano na kusaidiana

Elimu ina manufaa makubwa kwa watoto, familia zao na jamii kwa ujumla. Shule
zilizo salama zinaweza kusaidia mfumo wa elimu kufika malengo ya kutoa elimu
bora, afyabora, usalama na ulinzi na mahusiano mazuri.

Usalama shuleni huleta hamasa kwa watoto kujifunza na kuwajengea walimu uwezo wa
kumfundisha na watoto kuipenda shule. Afya na ustawi unachangiwa na hakuna fujo,
vurugu, matatizo ya tabia, hatari ya kimwili, hatari ya kihisia na hatari ya
kisaikolojia.

Usalama shuleni huchangia mahusiano mazuri kwa muingiliano mzuri kwa wanafunzi,
walimu,watenda kazi na jamii. Mahusiano mazuri husaidia ukuaji wa mwanafunzi
kihisia, kijamii na kiakili.

Kuhakikisha usalama wa mwanafunzi, mwalimu na mfanyakazi wengine shuleni.
Usalama wa mwanafunzi, mwalimu na wafanyakazi wengine itasaidia katika
ufundishaji wa kujifunza kwa kushirikisha walezi na jamii pia kuongeza
mahudhurio ya wanafunzi shuleni.

Utoaji wa elimu bora hufanyika kwa kuwashirikisha wazazi na jamii katika
kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi na wanahudhuria shuleni.
Kuhakikisha wanafunzi wanajifunza katika mazingira yasiyo  hatarishi na vitisho
yanayozingatia usalama wao ambazo utapelekea ufaulu mzuri.

Faida ya usalama shuleni inatengeneza mazingira mazuri ya kujifunzia, ambayo
mwanafunzi anajiona yupo salama na kupata msaada wa kutosha. Inahakikisha kila
mtoto anapata elimu kutokana na mahitaji yake maalum na kupata mazingira salama
ya kujifunzia.

Usalama shuleni una mbinu mbalimbali zenye kudhibiti ukatili na utayari ili
kuendeleza usalama wa mwanafunzi shuleni. Uongozi wa shule uanzishe mifumo na
mikakati ya wanafunzi kutoa maoni au malalamiko yao hii itawahakikishia
wanafunzi usalama wao na kutengeneza mazingira mazuri ya kujifunza.

Usalama shuleni hautalinda wanafunzi tu shuleni bali utawasaidia kukua kielimu
na binafsi.

Usalama shuleni utasaidia kumfanya mtoto awe salama shuleni, kwa kuwashirikisha
wadau wa elimu katika kutengeneza na kuendeleza mifumo ya usalama shuleni.
Kuongezeka kwa namba ya wanafunzi kuhudhuria shuleni na faida pia itaongezeka
katika jamii.

Usalama wa mwanafunzi shuleni ni msingi wa kuzingatiwa kwa kuchukua hatua
mbalimbali na ni lengo linaloweza kufikiwa




SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania27/09/202427/09/2024Posted inParentingLeave a comment
on MALEZI YA MTOTO NA USALAMA SHULENI


MALEZI YA MTOTO NA USALAMA NA ULINZI WA MTOTO

Kila familia, shule na jamii kwa ujumla inawajibu ya kuwapa watoto ULINZI na
kuhakikisha wako SALAMA. Ukiwa kama mzazi unawajibuwa kumlinda mtoto na
kumsikiliza lakini pia kumfundisha kujilinda yeye mwenyewe.

NAMNA YA KUONGEA NA WATOTO KUHUSU ULINZI NA USALAMA WAO

Mzazi anawajibu wa kumfundisha mtoto kuhusu usalama wake yeye mwenyewe. Mzazi
umfundishe ujuzi WA usalama kama vile kutumia akili kufikiria, kuwa na tabia ya
kujiamini hasa hisia zake na kushirikiana na watu wengine. Hakuna umri sahihi wa
mzazi kumfundisha mtoto usalama wake mwenyew anza sasa.

Mzazi msikilize mtoto wako ujue mambo yaliyokea katika siku yake mzima na tabia
zake. Msikilize mtoto nini anapenda nini hakipendi. Mfanye mtoto ajue kwamba
anaweza kuongea na wewe jambo lolote. Muhakikishie mtoto wako kwako ndio sehemu
salama linapotokea tatizo lolote.

MAMBO YAKUMFUNDISHA MTOTO YATAKAYO MSADIA USALAMA WAKE

Mwambie mtoto atambue mipaka sehemu za kwenda wanachoweza kuona na vitu vya
kufanya likitokea tatizo lolote. Mfundishe kujenga ujamaa asijitenge peke ake
sehemu hatarishi lakini pia ni sawa kusema hapana kama anaona kuna jambo halipo
sawa.



JUKUMU LA MZAZI KUHAKIKISHA USALAMA WA MTOTO

1. Lazima ujue mahali mtoto wako yupo mda wote

2. Mtoto akupe taarifa kama kuna tatizo lolote limetokea

3. Hakuna mtu mwingine anauepaswa kuwa makini na msimamia mtoto isipokuwa mzazi
mwenyewe

USALAMA WA MTOTO NYUMBANI

1. Mtoto anatakiwa ajue jina lake lote namba ya simu ya wazazi, nyumbani ata ya
mwanafamilia wa karibu

2. Kama mzazi haupo kuwa na mtu mzima anayeaminika ambaye mtoto anaweza kumpa
taarifa anapopata tatizo

3. Chagua dada wa kazi kwa uangalifu mkubwa, baada ya kumpata dada wa kazi
muulize mtoto wako maoni yake kuhusu dada wa kazi na usikilizekwa makini

4. Akague nyumba kwa nje kabla hajaingia, afunge milango, aite kujua kama kuna
watu ndani, asiwape taarifa watu nyumbani yupo mwenyewe na asifungue mlango kwa
mtu asiyemjua

USALAMA SHULENI

Mzazi kuwa makini na alama unazioekq kwenye vifaa vya shule vya mtoto vinaweza
kuhatarisha maisha yake . Kuhakikisha usalama wa mtoto anapoenda na kurudi
SHULENI. Jambo la msingi zaidi mtoto wako anapaswa kukwambia mambo yote
yaliyotokea shuleni kwake siku mzima.

MAMBO MUHIMU MTOTO ANAPASWA KUYAFAHAMU

1. Jina lake

2. Majina ya wazazi

3. Mahali anapoishi

4. Namba ya simu ya mzazi

5. Kumpa taarifa mzazi kabla hajaend sehemu yoyote au mtu yoyote

6. Kumpa taarifa mzazi au mtu mzima anayeaminika kabla hajapokea chochote ata
kutoka kwa mtu unayemfahamu

7. Acheze na marafik zake asicheze peke ake

8. Ni sawa kusema hapana kama anaona kuna jambo sio sawa, halielewi , linamnyima
raha, linamkosesha amani au amekatazwa

9. Lazima amamwambie mzazi au mtu mzima anayeaminika anapopatwa na tatizo lolote

10. Ana haki ya kuwa salama

ULINZI NA USALAMA WA MTOTO NI JUKUMU LA KILA MMOJA WETU NA JAMII KWA UJUMLA

TUWALILINDE WATOTO WETU




SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania24/07/202424/07/2024Posted inParentingLeave a comment
on MALEZI YA MTOTO NA USALAMA NA ULINZI WA MTOTO


MALEZI YA MTOTO YANAYOMPATIA FURAHA

Kila mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Furaha ya mtoto ni Jambo la muhimu ambalo
kila mzazi anatamani mtoto wake awe nayo.

Katika tafiti zilozofanywa katika nchi 67 duniani zenye tamaduni tofauti, imani
tofauti na vipato tofauti, wazazi kitu walichotamani kutokana na maswali
waliyoulizwa ni watoto wao kuwa na furaha.

Ni lazima kila mzazi aelewe huwez kufanya mtoto wako akawa na furaka, Ila
unaweza kufanya mambo yatakayo mtia nguvu aweze kuitafuta furaha yake yeye
mwenyewe. Jambo la kuzingatia wewe kama huwezi huwezi kufanya mtoto awe na
furaha isipokuwa unaweza kumtia mtoto nguvu kuitafuta furaha yake ya kweli yeye
mwenyewe.

Katika kumfanya mtoto awe na furaha mzazi anaweza kufanya nakosa ambayo
yakapelekea mtoto asiwe na furaha kwa mzazi kuamini kwamba anajua kilicho Bora
kwa mtoto wake.

Furaha ya kweli sio ile mtoto unayompatia bali ni ile atakayoitafuta mwenyewe
baada ya mzazi kumsaidia kwa kumpa nguvu kuipata furaha yake ya kweli.

Msaada wa mzazi ni mwanzo mzuri wa kumuwezesha mtoto kuwa na furaha ya kweli.
Tuwape msaada kutafuta furaha zao wenyewe tusiamini tunaweza kuwapa furaha. Kwa
kuongezea furaha za watoto hutofautiana tuzingatie hilo sana.

Kila analofanya mzazi ni hamu ya kuona mtoto wake anafuraha, hivyo tuwasaidie
watoto wetu kuitafuta furaha ya kweli wenyewe kwa kuwapenda. Tunavyowasaidia
watoto kutafuta furaha ya kweli malipo yake mzazi atapata furaha pia.

MALEZI NI FURAHA, FURAHIA KUWA MZAZI

KILA MZAZI ANATAKA MTOTO WAKE AWE NA FURAHA


SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania03/07/202424/07/2024Posted inParenting,
UncategorizedLeave a comment on MALEZI YA MTOTO YANAYOMPATIA FURAHA


MALEZI YA MTOTO MSICHANA (BALEHE)

Vijana wengi huingia katika balehe mapema sana, kuishi maisha ya kupendeza sana,
maisha ya vurugu, na ngono kwenye mitandao kuliko kizazi chochote kabla. Na bado
vijana wengi wa kike hawajakomaa vile watu wanavyofikiria. Ukuaji wao wa mwili
na mabadiliko ya haraka ulimwenguni. Kwa kuongezea huend shule muda mrefuu,
hivyo hawana uzoefu na majukumu ya watu wazima kuliko wasichana wakizamani.
Vijana wa kike huwa na tabia ya kuleta changamoto kwa mamlaka na kujilinganisha
na marafiki. Vijana wa kike huwa wachangamfu, wabunifu, wanajali na wasiri.
Lakini pia huitaji muongozo na msaada kutoka kwa wazazi, bibi na babu,
wanafamilia na washauri. Kuweka njia za mawasiliano wazi kunaweza kumsaidia
binti yako kuwa mkweli nini anachokifanya na kuhisi. Unaweza kumfanya mtoto
ajielezee kwa urahisi zaidi unapofanya nae shughuli kadhaa pamoja kama kuandaa
chakula, au kuosha vyombo au kuendesha gari. Zaidi ya hayo aina ya malezi
itabidi ibadilike wakati binti yako anajifunza kufanya maamuzi peke yake na
anakuwa zaidi. Vijana wengi kipindi huki hupitia machafuko makubwa ambayo
yinaweza kuacha makovu ya kudumu. Uzoefu wa maisha ya binti yako na mzazi wake,
mzazi wake huchukua sehemu kubwa. Mzazi zingatia utu wa mtoto wako, jambo la
mwisho mtoto wako anahitaji. Ikiwa hujashiriki kikamilifu binti yako kumbuka
haujachelewa sana kuanza.

MALEZI NI MALENGO


SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania11/06/202424/07/2024Posted inParentingLeave a comment
on MALEZI YA MTOTO MSICHANA (BALEHE)


MALEZI YA MTOTO NA MZAZI MMOJA NA FAMILIA ZA KILEO

Malezi Ya Mzazi Mmoja

Mzazi mmoja hulea mtoto/watoto bila msaada wa mwenzi, athari ya malezi ya mzazi
mmoja kwa mtoto inaweza kuwa nzuri au mbaya. Maisha katika nyumba ya mzazi
mmoja, japokuwa yamekuwa ni ya kawaida katika familia zetu za kileo yanaweza
kuleta msongo wa mawazo kwa mzazi na mtoto. Katika familia za kileo malezi ya
mzazi mmoja yamekuwa ya kawaida sana katika jamii zetu kuliko familia zenye
Baba, Mama na Watoto. Maisha katika nyumba zenye malezi ya mzazi mmoja yanaweza
kuleta msongo wa mawazo kwa mzazi na mtoto. Mzazi anaona amezidiwa na majukumu
ya kulea mtoto, kufanya kazi, kulipa bili mbalimbali,ada na kazi za nyumbani. Na
wakati mwingine vyanzo vya pesa hupungua pale mzazi anapobaki mwenyewe kulea
watoto. Familia zenye malezi ya mzazi mmoja mara nyingi hukutana na matatizo
mbalimbali ambayo yanaweza yasiwakute familia nyingine.

Matatizo yanayotokea kwenye familia ya malezi ya mzazi mmoja

Licha ya athari ambazo hutokana na malezi ya mzazi mmoja watoto wanaweza kuwa
wenye furaha na mafanikio. Kwa uangalifu zaidi, mzazi mmoja anaweza kulea mtoto
mwenye mafanikio na maendeleo bora ya jumla katika maisha yeao ya kijamii na
kihemko

 * Matokeo ya ugomvi unaoendelea kati ya wazazi wawili
 * Wazazi na watoto kukosa mda wa kujumuika kwa pamoja
 * Matokeo mabaya shuleni baada ya wazazi kutengana
 * Matatizo yanayotokea baada ya wazazi kuanzisha mahusiano mengine
 * Maelewano mabaya katika familia

Mzazi anayelea mtoto peke ake anaweza kusaidiwa na wanafamilia kwa kuongelea
hisia zao na kushilikiana kwa pamoja kutatua matatizo. Kupata msaada kutoka kwa
marafiki, wanafamilia na watu wa dini. Matatizo yakizidi ni salama kuwaona
madaktari wa afya ya akili.

Athari nzuri za malezi ya mzazi mmoja

Wakati unasikia juu ya athari mbaya ya malezi ya mzazi mmoja yanaweza kuwa
mazito, pia Kuna athari nzuri kwa watoto waliolelewa na mzazi mmoja

 * Mahusiano yalibora kati ya mzazi na mtoto
 * Kushiriki kwa pamoja katika majukumu ya familia
 * Mwingiliano wa uzoefu na jamii halisi
 * Ukomavu wa mzazi na mtoto kuhakikisha familia ipo vizuri

Malezi ni kazi ngumu. Wazazi wote kuna wakati wanakasirika na kufadhaika. Lakini
usitoe hisia zako juu ya mtoto wako. Ukianza kuhisi kuzidiwa, kuna vitu unaweza
kufanya ili usijisikie kuzidwa

 * Kubali msaada
 * Tafuta mda kwaajili yako na mtoto wako
 * Furahiya na mtoto wako
 * Tenga wakati kwaajili yako mwenyewe
 * Mtafutie mtoto watu wa kuwaiga kama mfano

Hata kama changamoto ni nyingi mzazi mmoja anaweza kulea mtoto mwenye mafanikio.
Muoneshe mtoto wako upendo, heshima na muonyeshe mambo chanya ya kuhakikisha
kuwa mtoto wako anastawi maishani

Unawezaje kudumisha afya yako akili kama mzazi mmoja?


SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania09/10/202124/07/2024Posted inParentingLeave a comment
on MALEZI YA MTOTO NA MZAZI MMOJA NA FAMILIA ZA KILEO


MALEZI YA MTOTO NA AFYA YA AKILI



Afya ya akili ya mtoto

Afya ya akili ya mtoto inamaanisha kufikia hatua ya maendeleo na ya kihemko na
kujifunza ujuzi mzuri wa kijamii na jinsi ya kukabiliana na wakati kuna shida

Afya ya akili ya mtoto ni nini?

Afya ya akili ya mtoto ni mtoto awe na hali nzuri ya maisha na aweze kufanya
kazi vizuri nyumbani, shuleni na katika jamii. Matatizo ya akili katika mtoto
zinaelezewa kama mabadiliko makubwa kwa njia ambayo mtoto hujifunza kawaida,
kuishii au kushughulikia hisia ambayo husababisha shida. Mara kwa mara mtoto
hupata hofu na wasiwasi au tabia ya kuvuruga. Ikiwa dalili ni mbaya na
zinaendelea na zinaingiliana na shule au shughuli za kucheza, mtoto anaweza
kugunduliwa na shida ya akili. Afya ya akili sio kutokuwepo kwa shida ya akili.
Mtoto ambaye hana shida ya akili anaweza kutofautiana katika jinsi anavyofanya
vizuri na mtoto aliye na ugonjwa huo wa akili uliogunduliwa anaweza kutofautiana
katika nguvu na udhaifu wao jinsi wanavyoendelea na kukabiliana, na katika
maisha yao. Afya ya akili kama na kitambulisho cha shida maalum za akili ni njia
zote mbili za kuelewa jinsi mtoto anavyofanya vizuri

Je! Ni shida gani ya kawaida ya akili ya mtoto

Miongoni mwa shida za kawaida za akili zinaweza kugunduliwa katika utoto ni
shida ya umakini, wasiwasi na shida ya tabia. Matatizo mengine ya mtoto na
wasiwasi huathiri mtoto anavyojifunza, kuishii au kushughulikia hisia zake
zinaweza kujumuisha ulemavu wa ujifunzaji, usonji na sababu za hatari kama
matumizi ya dutu na kujidhuru

Je! Ni nini dalili za shida ya akili ya utoto

Dalili za shida ya akili ya mtoto hubadilika mtoto anavyozidi kukua, na anaweza
kujumuisha shida na jinsi mtoto hucheza, anajifunza, huongea na vitendo au jinsi
mtoto anashughulikia hisia zake. Dalili mar nyingi huanza katika utoto wa mapema
ingawa shida zingine zinaweza kutokea wakati was ujana. Utambuzi hufanywa mara
nyingi katika miaka ya shule na wakati mwingine mapema hata hivyo watoto wengine
wenye shida ya akili inaweza isitambuliwe

Je! Shida za akili za utotoni zinaweza kutibiwa

Shida za akili za utotoni zinaweza kudhibitiwa na kusimamiwa. Kuna chaguzi
nyingi za matibabu kulingana na ushahidi wa matibabu na was kisasa. Mzazi na
madaktari wanapaswa kufanya kazi kwa ukaribu na kila mti anayehusika na matibabu
ya mtoto, walimu, makocha , mtaalamu na wanafamilia wengine. Kuchukua faida ya
rasilimali zote zinazopatikana itasaidia wazazi, wataalamu wa afya na
waelelimishaji wamuongoze mtoto kuelekea mafanikio. Utambuzi wa mapema na huduma
zinazofaa kwa watoto na familia zao zinaweza kuleta mabadiliko katika maisha yao
ya watoto na shida ya akili

Nani huathirika?

Shida ya akili ya mtoto huathiri watoto na familia nyingi. Wavulana na wasichana
wa miaka yote, makabila yote na duniani kote kupata shida ya akili

Je! Ni athari gani ya shida ya afya akili kwa mtoto

Afya ya akili ni muhimu kwa afya ya jumla. Shida ya afya ya akili ni hali ya
kiafya sugu- Hali ambazo hudumu kwa muda mrefu na mara nyingi haziendi kabisa
ambazo zinaweza kuendelea kwa muda wa maisha. Bila utambuzi wa mapema na
matibabu, mtoto aliye na shida ya akili anaweza kuwa na shida nyumbani, shuleni
na kutengeneza urafiki. Matatizo ya akili pia yanaweza kuingilia kati ukuaji
mzuri wa mtoto, kusababisha shida ambazo zinaweza kuendelea adi utu uzima.
Kusaidia afya ya akili ya watoto pamoja na;

 * Kuhakikisha watoto wanatimiza hatua za maendeleo
 * Kuelewa nini cha kufanya wakati kuna wasiwasi
 * Kusaidia mkakati mzuri wa uzazi
 * Kuboresha upatikanaji wa huduma

Unaweza kufanya nini!

1. Wazazi

Mzazi unamjua mtoto wako vizuri zaidi. Ongea na mtaalamu wa utunzaji wa mtoto
wako ukiwa una wasiwasi juu ya njia ya mtoto wako nyumbani, shuleni au marafiki

2. Vijana

Ni muhimu kutunza afya yako ya akili kama vile kutunza afya yako ya mwili, ikiwa
umekasirika, wasiwasi na huzuni. Usiogope kuzungumza juu ya hisia zako na
wasiliana na mtu mzima au rafiki

3. Mtaalamu wa matibabu

Utambuzi wa mapema na matibabu sahihi kulingana na miongozo iliyosasishwa ni
muhimu sana. Kuna rasilimali zinazopatikana kusaidia kugundua na kutibu shida ya
akili ya watoto

4. Walimu/ Wasimamizi wa shule

Utambuzi wa mapema ili watoto waweze kupata msaada wanaohitaji. Fanya kazi na
familia ma wataalamu wa huduma ya afya ikiwa una wasiwasi juu ya afya ya akili
ya mtoto katika shule yako

> Je! waijua

Siku ya afya akili ya watoto?


SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania07/06/202124/07/2024Posted inParentingLeave a comment
on MALEZI YA MTOTO NA AFYA YA AKILI


MALEZI YA MTOTO NA UNYANYASAJI WA WATOTO

Unyanyasaji wa watoto

Unyanyasaji wa watoto ni vitendo vya unyanyasaji na kupuuzwa vinavyotokea kwa
watoto chini ya miaka 18. Inahusisha vitendo vyote vya unyanyasaji wa kimwili,
kihisia, kijinsia, kupuuzwa, uzembe, kibiashara na unyonyaji mwingine ambayo
hupelekea uhalisia wa madhara kwa afya za watoto, kuishi heshima, mahusiano
majukumu, majukumu, uaminifu na nguvu

Ukubwa Wa Tatizo La Unyanyasaji Wa Watoto

Unyanyasaji wa watoto ni tatizo la duniani kote na huleta athari mbaya katika
maisha. Japokuwa tafiti nyingi zimefanywa bado nchi nyingi hazina idadi kamilifu
ya vitendo vya unyanyasaji wa watoto. Unyanyasaji wa watoto ni ngumu sana
kufanyia utafiti, kwa sababu kila nchi ina namna yake ya kufanya utafiti
kutegemea na

 * Maana ya unyanyasaji wa watoto inavyotumika
 * Aina ya unyanyasaji wa watoto inavyofanyiwa utafiti
 * Ubora wa takwimu
 * Ubora wa utafiti

Bila kikomo tafiti nyingi zimeonyesha kwamba karibia watoto wa 3 katika watoto
wa 4 kati ya miaka 2 mpaka 4 hupata adhabu za kimwili au mvurugo wa kisaikolojia
katika mikono ya wazazi au walezi na imeripotiwa kati ya wanawake 15/13 wanaume
mmoja alipata manyanyaso ya kijinsia wakati wa utotoni

Kila mwaka, inakadiriwa katika kifo cha mauaji kwa watoto chini ya miaka 18
hutokana na unyanyasaji wa watoto

Matokeo Ya Unyanyasaji Wa Watoto

Unyanyasaji wa watoto husababisha mateso kwa mtoto na familia na inaweza kuwa na
athari mbaya katika maisha. Unyanyasaji wa watoto husababisha msongo wa mawazo
inayohusishwa na uharibifu was ukuaji wa akili katika umri mdogo. Msongo wa
mawazo uliozidi inaweza kudhoofisha ukuaji wa mfumo wa neva na kinga. Watu
wazima waliopata unyanyasaji utotoni wako katika hatari zaidi ya tabia, mwili na
matatizo ya afya ya akili kama:

 * Huzuni
 * Kuvuta sigara
 * Unene kupita kiasi
 * Tabia hatari za ngono
 * Ujauzito usiokusudiwa
 * Pombe na matumizi ya dawa za kulevya
 * Magonjwa ya moyo
 * Kansa
 * Kujiua
 * Maambukizi ya zinaa

Ukatili dhidi ya watoto ni sababu moja wapo inayopelekea kutokuwa na usawa
katika elimu, zaidi ya matatizo ya afya, jamii na elimu kuna athari za kiuchumi
kama: matibabu ya kiafya

Sababu Za Athari

1. Wazazi/Walezi

Ni muhimu sana kusisitiza kwamba watoto ni wahanga na haipaswi kuwabebesha
lawama za unyanyasaji wa watoto

Sifa za mtoto ambaye anaweza kupata manyanyaso

 * Mtoto kuwa chini ya miaka 4 au balehe
 * Mtoto kushindwa kutimiza matarajio ya mzazi
 * Mtoto mwenye mahitaji maalum, anayelia sana au kuwa na kasoro za kimwili
 * Kumuona mtoto yupo sawa na jinsia ya tofauti na yake au kuwa na jinsia mbili

Sifa za mzazi/mlezi ambaye anaweza kuongeza uwezekano was mtoto kufanyiwa
unyanyasaji

 * Mzazi/mlezi hawezi kutengeneza mahusiano mazuri na mtoto
 * Mzazi/mlezi aliyepitia manyanyaso utotoni
 * Mzazi/mlezi hana uelewa na ukuaji wa mtoto
 * Mzazi/mlezi kutumia pombe kupita kiasi na matumizi ya dawa za kulevya
 * Mzazi/mlezi asiyeweza kujizuia hasira
 * Mzazi/mlezi mwenye matatizo ya akili
 * Mzazi/mlezi anayejihusisha na vitendo vya uhalifu
 * Mzazi/mlezi mwenye matatizo ya kifedha

2. Mahusiano

Tabia za mahusiano katika familia, marafiki na watu mbalimbali tunaoingiliana
nao katika maisha inaweza kuongeza uwezekano wa mtoto kupata unyanyasaji

 * Kuvunjika kwa familia
 * Kutengwa katika jamii
 * Kuvunja usaidizi wa ndugu na jamaa katika malezi ya mtoto

3. Jamii

Sifa za jamii zinazoweza kuongeza hatari ya unyanyasaji wa mtoto ni pamoja na:

 * Usawa wa kijinsia wa jamii husika
 * Ukosefu wa nyumba za kutosha
 * Kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira na umaskini
 * Upatikanaji rahisi wa pombe na dawa za kulevya
 * Sera na mipango isiyotosheleza kuzuia unyanyasaji wa watoto, upigaji picha za
   watoto,ukahaba wa watoto na ajira ya watoto
 * Kanuni za kijamii na kitamaduni zinazokuza unyanyasaji wa watoto
 * Sera za jamii, kiuchumi, kiafya na elimu zinazopelekea maisha duni

Kuzuia unyanyasaji wa watoto

Kuzuia na kuwajibika katika unyanyasaji wa watoto inahitaji mbinu ya kitabaka(
ushirikiano wa wa wadau). Uingiliaji huo wa mapema hufanyika katika maisha ya
watoto, huleta faida kubwa kwa mtoto na jamii

Uingiliaji mzuri na wa kuahidi ni pamoja na:

 * Usaidizi wa wazazi na walezi
 * Mbinu ya elimu na stadi za maisha
 * Kanuni na njia za kuthamini
 * Utekelezaji na uimarishaji wa sheria
 * Majibu na huduma za msaada

Tuache Unyanyasaji Wa Watoto

TUACHE


SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania08/05/202124/07/2024Posted inParentingLeave a comment
on MALEZI YA MTOTO NA UNYANYASAJI WA WATOTO


6. MALEZI YA MTOTO WA VIJANA( BALEHE)

Vijana

Ujana ni kipindi cha kati ya utoto na ukubwa, huanzia miaka 12 mpaka 18. Vijana
hupata mabadiliko ya mwili ambayo huashiria kuwa mkubwa

Ukuaji wa mwili

Mabadiliko haya yanaweza kuwa ya kuchanganya na saa nyingine kutisha. Ni muhimu
sana kwa mzazi kufahamu ni mabadiliko gani mtoto huyapata anavyokuwa katika
ujana

Mabadiliko kwa wavulana

 * Mabadiliko ya homoni ambayo hupelekea mabadiliko ya mwili katika sehemu za
   siri za kiume
 * Kuota nywele kwenye makwapa, sehemu za siri, kifuani na usoni
 * Mabega kuwa mapana
 * Sauti huanza kubadilika na kuwa nzito

Mabadiliko kwa msichana

 * Mabadiliko ya homoni huandaa mwili wa msichana kuanza kupata hedhi
 * Kuota nywele chini ya makwapa na sehemu nyingine za siri
 * Mwili kaanza kubadilika na kuwa mkubwa wenye shepu kubwa na matiti kuota

Matokeo ya mabadiliko

 * Mabadiliko hupelekea ngozi kuwa na mafuta mengi ambayo hupelekea chunusi
   kwenye ngozi ya kijana
 * Mabadiliko hupelekea matatizo ya kutokujiamini kwa kijana

Jamii na muonekano wa mwili wa kijana

 * Upatikanaji wa habari kwa urahisi unaweza kumuathiri kijana kuhusu muonekano
   wake ( mabadiliko) kwenye mwili wake. Mfano; kutaka kuwa kama muigizaji
   fulani
 * Kujiringanisha katika jamii na kutaka kuwa kama mtu fulani kwenye jamii
   inayomzunguka
 * Kuonewa na kutaniwa humshusha mtoto uwezo wake wa kujiamini

Usaidizi wa mzazi

Mzazi anatakiwa azungumze na mtoto na ajaribu sana mazungumzo yawe chana. Mpatie
mtoto pongezi na majadiliane kwa pamoja mafanikio, wakati wa maongezi mzazi
atambue mawazo hasi na amsaidie mtoto ayaone ni chanya. Mzazi msifie mtoto kwa
usahihi ampongeze na kumhimiza. Mzazi msaidie mtoto kuelewa mabadiliko ya mwili
wake ambayo hawezi kuyabadilisha yeye. Mzazi hata siku moja asimfananishe mtoto
na uwezo wake na marafiki zake, hii inaweza kuwa hatari kwa mtoto akihisi hana
uwezo kama marafiki zake

Uwezo wa utambuzi

Kijana anakuwa na uwezo wa kuwaza na kujiandoa. Anauwezo wa kufikiria kwa dhana,
kuzingatia uwezekano na kimantiki. Kijana huchukua mitazamo na kuelewa lakini
pia kuzingatia mitazamo mingine. Kijana hujiekea zaidi malengo, ukuaji wa akili
ya kijana mara nyingi huathiriwa na hali yake ya hisia. Kijana huanza kuelewa
sura za ulimwengu wa watu wazima

Mahitaji ya kihemko ya kijamii

Kijana huitaji kutengeneza uhuru wake yeye mwenyewe, lakini pia kujumuika na
jamii kwa kiwango kikubwa huka ikiwa ni matarajio makubwa na mahitaji. Kijana
kutafuta kukubalika katika kundi la marafiki zake, hufanya maamuzi yake peke ake
na yuko tayari kusema hapana. Kijana hujaribu kutengeneza umaarufu wao na sio
kutegemea wazazi (Hii inaweza kupelekea ugomvi na wazazi). Kijana huanza kuwa
karibu zaidi na marafiki kuliko wazazi kwa ajiili ya msaada, kuanza kujihusisha
na mahusiano ya kimapenzi. Kijana anaweza kumudu hisia zake na kuanza kujikubali

Matatizo yanayoweza kujitokeza

 * Kijana kupata msongo wa mawazo uliopitiliza
 * Kijana anaweza kujitenga na makundi ya marafiki asiyoendana nayo na kujiweka
   pamoja na makundi anayofanana nayo
 * Kijana kutoweza kujihusisha na masomo

Malezi mazuri

Kijana asaidiwe kuweka malengo yake ya baadae, lakini pia afundishwe jinsi ya
kushughulikia mahusiano na kijana wa jinsia nyingine. Kijana apewe nafasi ya
kushughulikia maisha yake ya siri. Apewe kazi mbalimbali ili azitumie nguvu zake
kwenye kazi za maana

Malezi mabaya

 * Tusiwalee vijana kama watoto wadogo
 * Tusiwape uhuru uliopitiliza vijana
 * Kutomsaidia kijana kujua malengo yake ya baadae

> Katika malezi ya mtoto malengo ya mzazi kwa mtoto wake ni muhimu sana, huamua
> utu uzima wa mtoto
> 
> Parenting Tanzania


SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania11/04/202124/07/2024Posted inUncategorizedLeave a
comment on 6. MALEZI YA MTOTO WA VIJANA( BALEHE)


5. MALEZI YA MTOTO WA UMRI WA SHULE

Umri wa shule

Katika kipindi hiki ambacho mtoto ana miaka 3 mpaka 6-7, ukuaji wa mtoto katika
kipindi hiki huwa ni mdogo kwasababu nguvu nyingi hutumika katika kupata maarifa
kuliko kuongezeka kwa mwili

Ukuaji wa mwili

Urefu huongezeka takribani 5cm kwa mwaka. Mtoto (kike/kiume) huwa na miguu
mirefu.

Harakati na vitendo vya misuli

Mtoto wa umri wa shule huanza kuona maendeleo yao katika harakati na vitendo vya
misuli. Watakuwa vizuri zaidi katika kudhibiti, kuratibu na usawa. Misuli yao
huanza kubadilika katika watoto wa umri wa shule ambayo huwafanya wawe na nguvu
za kutosha

Hatua kuu za ujuzi wa kazi

 * Uwezo mkubwa wa harakati na vitendo vya misuli
 * Hisia za ukuaji wa mwili hukua
 * Kujua mwili wake unakimbilia balehe
 * Utofauti wa jinsia hujionyesha

Ukuaji wa akili

Mtoto wa umri wa shule huwa na uwezo wa kuelewa mantiki na habari halisi hasa
katika maisha yake binafsi. Mtoto anaweza bado akapambana kufahamu dhana ya
kudhani/kufikirika hasa kwa zile zitakazotokea katika kipindi kirefu kijacho.
Mtoto wa umri wa shule huanza kufikiria watu wengine na kuwa na uwezo wa
kufikiria na kuelewa vitu kutoka katika maoni mbalimbali

Kazi za utambuzi

Mtoto wa umri wa shule anakuwa na uwezo wa kuzingatia kazi/mada. Mtoto ataanza
pia kudharau usumbufu wowote wanapokuwa na kazi/mada ya kuzingatia. Uwezo wa
kutunza kumbukumbu kwa mda mrefu au mfupi huanza kuimarika katika kipindi hiki
cha umri wa shule. Mtoto wa umri wa shule atakuwa na uwezo wa kuvuta kumbukumbu
ya vitu muhimu ( vilivyotokea miezi au miaka iliyopita). Mtoto huwa na uangalizi
mzuri, anakuwa na uwezo wa kuzingatia kazi kazi muhimu kwa muda mrefu. Mtoto
huanza kusoma vitabu vyenye kurasa nyingi, kuwa na vitu anania navyo shuleni na
kujihusisha katika miradi ya muda mrefu

Kuchochea kwa Utambuzi

Kuchochea kwa utambuzi katika kipindi cha umri wa shule, mzazi ampe mtoto vitu
chochezi katika utambuzi na michezo yenye changamoto. Mtoto apewe vitabu vingi
mbalimbali vyenye makuzi sahihi na tamaduni mbalimbali. Mzazi awe mfano wa
kuonyesha umuhimu wa kujali, heshima, ukweli na majukumu. Mtoto apewe nafasi
ambayo mtoto wa umri wa shule atapumzika na apewe uhuru mda huo atafanya nini.
Mzazi atekeleze shughuli ambazo zitafanywa kwa pamoja zinazoweza kutumia nguvu
na uwezo

Hatua za kihemko katika jamii

Umri wa shule mtoto huingiliana na jamii tofauti na nyumbani ambapo hupelekea
maadili yanayopingana, japokuwa mtoto huwa makini na yeye mwenyewe hujifunza kwa
bidii na kugundua ni kwa jinsi gani watu wanaozunguka huwasaidia katika kukua na
kujifunza ( mtoto hujiringanisha na kuchagua marafiki). Maoni hasi ya marafiki
huweza huleta kizuizi kikubwa

Mahitaji ya kihemko ya kijamii

Mtoto katika kipindi cha umri wa shule,huanza kujiuliza maswali kama yeye ni
nani? Nani anampenda? Mtoto huanza kutambua historia ya familia yake na
kuendelea kuelewa yeye ni nani. Mtoto hufanyia kazi suala la maadili na imani
lakini pia kuchukua misimamo. Mtoto huanza kujitegemea yeye mwenyewe , mtoto wa
umri wa shule hutafuta hongera kutoka kwa watu wazima pale wanapofanya vizuri.
Mtoto huwa na wivtu kwa ndugu yake au rafiki ake anayefanya vizuri kumzidi yeye
au anayeonekana zaidi kwa wazazi au mtu mzima yoyote

Malezi mazuri ya mtoto

Mzazi mzuri humsaidia mtoto kujiona Hana shida na anapata msaada, kugundua mambo
mazuri ambayo mtoto ameyatimiza. Mzazi humueshimu mtoto na kumsikiliza
anachokisema na kuyatendea kazi vitu mtoto anavyovipenda, kumkubali na kumpatia
hongera. Mzazi mzuri huwa mkweli na hufuatilia anachokisema atakifanyia kazi,
lakini pia mzazi humsaidia mtoto kutengeneza mahusiano mazuri na rafiki zake.
Mzazi pia anapaswa kumfundisha mtoto kuziendesha hisia zake, kumsaidia kuepuka
msongo wa mawazo wakati anatengeneza urafiki

Je! wajua kuwa katika malezi ya mtoto wako lazma uwe na malengo?


SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania11/04/202124/07/2024Posted inUncategorizedLeave a
comment on 5. MALEZI YA MTOTO WA UMRI WA SHULE


4. MALEZI YA MTOTO KATIKA UMRI WA UTOTO WA MAPEMA

Utoto wa mapema

Utoto wa mapema ni kipindi kati ya miaka 4 adi 7. Ni kipindi ambacho mtoto
hupata elimu yake ya awali ( chekechea)

Ukuaji wa mwili

Mtoto katika kipindi hiki huongezeka takribani kilo 1.8 kila mwaka na urefu wa
mtoto huongezeka

Muonekano wa mwili

Mtoto huwa mrefu na mwili hupungua ukilinganisha na mtoto mdogo. Miguu yake na
sehemu nyingine za mwili huendelea kukua, kichwa chake huwa kidogo ukilinganisha
na mwili wake

Harakati na vitendo vya misuli

Harakati na vitendo vya misuli katika kipindi hiki ni matokeo ya maendeleo ya
mwili wa mtoto. Mtoto mwili unavyoendelea kukomaa pia huendelea kuimarisha
misuli yake na uwezo wa kudhibiti mwili wake vizuri

Ujuzi katika maisha

Mtoto anakuwa katika harakati za kila wakati, harakati na vitendo vya misuli ni
vya kusudi zaidi. Mtoto hutumia muda mwingi katika shughuli za mwili kama vile
kukimbia, kupanda vitu mbalimbali, kuruka na kukimbia

Hatua kuu za utoto wa mapema

 * Aweze kutumia uma na kijiko
 * Aweze kubembea na kuponda vitu
 * Aweze kuruka vitu

Kusisimua kwa mwili (Utoto wa mapema)

Mzazi mruhusu mtoto acheze lakini katika mazingira yaliyo salama kwa mtoto.
Tumuangalie mtoto anapokuwa anacheza na uhakikishe unajumuika katika michezo
yake. Muache mtoto azunguke na achunguze ili akuze maendeleo ya hisia. Walimu
wahakikishe kwamba darasa linahusisha harakati za mwili

Kujifunza kwa mtoto ( Utoto wa mapema)

Mtoto katika kipindi hiki hujifunza kwa kupitia kugundua, kuchunguza, majaribio
na kutatua matatizo

Uwezo wa utambuzi

Mtoto wa shule ya awali huanza kuona vitu kutokana na mtazamo wa watu wengine na
huanza kuelewa jinsi tabia zao zinavyoathili watu wengine. Mtoto anaendeleza
ujuzi wake wa lugha ya mdomo, kupata misamiati mipya na muundo wa sentesi. Mtoto
anaelewa dhana ya nafasi,mda na vipimo lakini pia dhana kama jana, leo na kesho.
Mtoto anajua kushoto na kulia. Mtoto huanza kukuza hali ya kujiamini na uwezo wa
kujifunza. Mtoto hujifunza kusema na kuandika na anauwezo wa kutamka maneno
rahisi. Mtoto anaanza kujadili na kubishana, anauwezo wa kufanya hesabu rahisi

Kusisimua utambuzi (Utoto wa mapema)

Tuwe mfano kwa mtoto, mtoto hufanya yale wanayotuona tunafanya. Mtoto aulizwe
maswali ya wazi anayoweza kuelewa. Mtoto apatiwe vifaa kumtia moyo kutatua
matatizo na ugunduzi

Maendeleo ya kihemko ya kijamii

Maendeleo ya kihemko ya kijamii katika hiki kipindi inahusisha mtoto kujitegemea
katika vitu kama mazoea, kushilikiana na wenzake, kujua maana ya uhusiano na
watu wengine, kudhibiti hisia na kukuza muonekano wake binafsi. Saikolojia
inasema mtoto katika hiki kipindi humpenda zaidi mzazi wa jinsia tofauti tofauti
na yake, kumsaidia mtoto kufafanua jinsia yake. Mtoto hupata upendo wake wa
kwanza na jinsi ya kushughulikia mapenzi kwa kina

Hatua za kihemko za kijamii

Mtoto hukuza uelewa wa huruma, kutengeneza na kutunza mahusiano mazuri na
urafiki. Mtoto anaanza kukuza hali ya maadili lakini pia kutambua na kusimamia
hisia zake. Mtoto hutengeneza mtazamo chana wa kujitambua yeye mwenyewe na maoni
kuhusiana na maadili na kujifunza baya na zuri, mtoto anakuwa na uwezo wa
kuonyesha mtazamo wake na majadiliano ya mtazamo wake. Mtoto anaanza kuelewa
mambo mbalimbali yanayo mzunguka na hata kuigiza maswali kuhusu kifo. Mtoto
hukubali kwamba wazazi sio watu wenye nguvu mda wote. Mtoto atataka kuwaomba
msamaha marafiki zake, kukubali na sheria zinazowekwa, kupenda kuimba , kucheza
mziki na kuigiza, kujua maana ya jinsia yake na kuweza kusema lipi ni la kweli
pamoja na vitu vinavyoweza kukuaminisha

Umuhimu wa hatua za kihemko za kijamii

Hatua za kihemko za kijamii ni za muhimu sana kwa mafanikio ya mtoto shuleni na
nyumbani na ukuaji wa mtoto kwani ujumla

Matatizo ya kihemko ya kijamii

 * Kushindwa shule
 * Kukosa marafiki
 * Kujitenga na jamii
 * Kuwa na aibu
 * Kutaka kuwa na nguvu

Mzazi muwajibikaji

Mzazi muwajibikaji katika kipindi hiki hutatua matatizo ya mtoto na kumsaidia
kuongelea hisia zao pamoja na wenzao. Mzazi kumuelewa mtoto na kumsaidia kuwa
karibu na mzazi wa jinsia nyingine lakini pia ni mda mda wa kuwaelekeza katika
maadili mazuri. Mzazi amsaidie mtoto mtoto kuweza kuzuia hisia za zake na kujua
umuhimu wa kuanzisha mipaka (heshima). Mzazi amruhusu mtoto kucheza na watoto
wengine na kumpatia vitu vya kuchezea vitakavyokuwa msaada katika ukuaji. Mzazi
acheze pamoja na watoto na kuangalia kwa ukaribu michezo wanayocheza. Mzazi
afuate muongozo wa mtoto, ampe msaada vitu mtoto anaufahamu navyo na kujifunza

Malezi mabaya

 * Lugha ya matusi kwa mtoto
 * Upendeleo wa mtoto
 * Ubaguzi wa

> Malezi ni malengo
> 
> ParentingTanzania




SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania11/04/202124/07/2024Posted inUncategorizedLeave a
comment on 4. MALEZI YA MTOTO KATIKA UMRI WA UTOTO WA MAPEMA


3. MALEZI YA MTOTO KATIKA UMRI WA UTOTO MDOGO

Utoto mdogo

Kipindi cha utoto mdogo ni kati ya mwaka 1 adi 3. Wakati wa kipindi ukuaji wa
mtoto huwa mdogo kuendana na mtoto

Kutokana na uwezo wa mtoto kutembea, mtoto anauwezo wa kutoka sehemu moja kwenda
kwingine. Hi huthibitisha njia ya uchunguzi na kujifunza mazingira yao

Hatua kuu kipindi cha utoto mdogo

 * Anatembea mwenyewe
 * Anasaidia kuvua nguo mwenyewe
 * Anatumia vyombo vya kulia chakula
 * Anaanza kukimbia
 * Anaweza kuchora mistari na maduara

Maendeleo ya utambuzi

Mtoto mdogo hutumia akili na misuli mikubwa kujitofautisha na vitu. Katika
kipindi hiki mtoto hutengeneza mantiki japokuwa atahangaika, atakua na mitazamo
tofauti, uanishaji na kuona umuhimu wake binafsi

Uwezo wa utambuzi

Mtoto mdogo katika uwezo wa utambuzi huweza kutofautisha maumbo na rangi,
anaweza kuchezea vitu vya kuchezea, kucheza michezo rahisi, kuchora maduara na
penseli, kufungua kurasa za vitabu, anatumia lugha kuelezea mawazo na hisia zao
na kutumia ujuzi wa kufikiri kutatua matatizo

Ishara za hatari kipindi cha utoto mdogo

 * Hanakili wengine
 * Hawezi kuonyeshea vitu
 * Ujuzi mdogo wa utendaji
 * Hafuati maelekezo rahisi
 * Hupoteza ujuzi alioupata

Mahitaji ya kihemko ya kijamii

Mategemeo ya hatua kuu ya mahitaji ya kihemko ya kijamii huendeshwa na maadili
ya kitamaduni na upendeleo. Watu wazima hushiriki maadili ya kitamaduni na imani
pamoja na mtoto kupitia mwingiliano wa kila siku

Kila mtoto huzaliwa na njia ya kipekee ya kuukaribia ulimwengu. Mfano; Mtoto
anaweza kua na harakati wakati mwingine hukaa na kuangalia dunia inayomzunguka.
Baada ya kujua kila mtoto mdogo huwa wa kipekee huna budi kuhimiza juhudi zake
na kumsaidia mahitaji yake. Mtoto mdogo huona fahari kwa msaidizi wake
anapoonyesha uwezo wake

Wasiwasi na Mgeni

Mtoto mdogo huonyesha kusumbuliwa na uwezo wa mgeni. Mtoto asipoonyeshwa
kusumbuliwa na uwepo wa mgeni anakua katika hatari ya unyanyasaji

Mtoto mdogo kuwa mkali

Mtoto mdogo hupinga mamlaka kwasababu ya kuhisi kutoeleweka au kusikilizwa.
Kuelewa tatizo la mtoto na mazungumzo inaweza kusaidia kupunguza ukali wa mtoto

Mashindano ya ndugu

Mtoto huwa na tabia ya fujo au kumuonea wivu ndugu yake. Kilele ni kati ya mwaka
1 hadi 2 lakini inaweza kuendelea muda mrefu bila kikomo

Mzazi anawezaje kukabiliana nayo?

 * Msifie mtoto kwa tahadhari, tumfikirie mtoto ambaye hafanyi vizuri
 * Mzazi uwatendee watoto sawa

Mtoto mdogo kunyonya vidole

Tabia ya mtoto kunyonya vidole vyake mara kwa mara, huonyesha kwamba mtoto hana
furaha. Mtoto mdogo huihisi hali ya kihemko ya mzazi,mtoto mdogo hujiona yupo
mpweke wanapohisi kuna kitu hakipo sawa

Mzazi mzuri

Mzazi mzuri humsaidia mtoto mdogo kujiona yupo salama, anastareheka na mdadisi

 * Tujibu vidokezo vya kumjengea uaminifu
 * Sisitiza utaratibu na uchunguzi
 * Tuwasaidie kutatua matatizo
 * Tengeneza tabia ya kujali na huruma katika kila kitu unachofanya na mtoto
   mdogo
 * Msomee mtoto mdogo vitabu na muonyeshe picha za hisia mbalimbali
 * Tengengeneza uhusiano mzuri na familia pamoja na mtoto mdogo

Wazazi hufikilia nini hasa kuhusu malezi ya mtoto mdogo?


SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania03/02/202124/07/2024Posted inUncategorizedLeave a
comment on 3. MALEZI YA MTOTO KATIKA UMRI WA UTOTO MDOGO


2. MALEZI YA MTOTO KATIKA UMRI WA UTOTO

Utoto

Kipindi hiki huanza mwezi wa kwanza mpaka mtoto anapofikisha mwaka mmoja. Ukuaji
na maendeleo ya mtoto katika kipindi hiki huwa ni haraka

Maendeleo ya mwili

Maendeleo ya mwili wa mtoto ni uwezo wa mtoto kutumia na kudhibiti mwili wake.
Maendeleo ya kimwili yaendane na ukuaji wa mtoto na kukua kwa ujuzi wa mwili
ikiwa ni pamoja na akili, misuli na akili. Mfano ; Watoto hujifunza dunia yao
wanapo ona, shika, kunusa, kusikia na ladha

Hatua kuu za utotoa

 * Anashikila kichwa thabiti
 * Anarefuka
 * Anakaa chini
 * Anatambaa
 * Anasimama mwenyewe
 * Anatembea mwenyewe

Kichochea maendeleo ya mwili wa mtoto

Wazazi ili kusaidia maendeleo mazuri ya mwili wa mtoto, tumsaidie mtoto kwa
kushikilia mwili na kichwa tunapowashika. Tuwasaidie watoto kuona sura zetu
tunapoongea na kucheza nao. Tuwape nafasi ya kujifunza na kutumia ujuzi kama
kukaa chini huku akimsaidia shingo yake na mgongo. Wazazi waeke vitu karibu na
kuwapa nafasi watoto ya kufikia vitu. Watoto watengenezewe mazingira salama
kwaajili ya kutambaa na kujifunza vitu mbalimbali. Wazazi wampe mtoto vitu vya
kuchezea vitakavyomsaidia mtoto katika maendeleo ya mwili wake

Watoto huzaliwa na matendo yasiyo ya hiyari, matendo hayo hufurahisha watoto
wanapoyafanya. Wanapokuwa wakubwa matendo hayo hupotea

 1. Mtoto anafungua mdomo kwaajili ya kunyonya wanapohisi Kuna kitu karibu ya
    mdomo
 2. Mtoto anaposhika kitu vizuri kwa mkono wake
 3. Mtoto anatupa miguu, mikono na kichwa huku analia
 4. Mtoto anapojikunja mwili wake anaposhika kwa vidole mgongoni au miguuni

Uwepo wa vitendo hivi kwa mtoto ni muhimu sana, ni ishara ya maendeleo ya mfumo
wa neva kufanya kazi vizuri

Dalili/Ishara kuharibika maendeleo ya mwili wa mtoto

 1. Mtoto hawezi kutupa mikono
 2. Mtoto hawezi kusimamisha shingo
 3. Mtoto anamiguu na mikono migumu/dhaifu
 4. Mtoto hawezi kukaa chini au kutambaa
 5. Mtoto hawezi kujilisha mwenyewe

Maendeleo ya utambuzi ( Utoto)

Katika hatua ya utoto mtoto hutumia akili, ukuaji wa mwili na uwezo wa kushika
vitu humsaidia mtoto kujitofautisha na vitu

Uwezo wa utambuzi (Utoto)

Vitendo mtoto anatakiwa afanye kuonyesha anauwezo wa utambuzi (mtoto akiwa na
miezi 6)

 * Mtoto anatambua sura anazozifahamu na kujua sura ambazo hazifahamu
 * Mtoto anapenda kucheza na wengine, hasa wazazi
 * Mtoto hujibu hisia za wengine na kufurahia
 * Mtoto anapenda kujiangalia mwenyewe katika kioo
 * 

Mzazi mzuri

Mzazi mzuri humsaidia mtoto katika ukuaji wake kwa kufanya yafuatayo;

 * Muoneshe/fanya unachotaka mtoto akifanye
 * Muhimize mtoto acheze
 * Muhimize mtoto katika kutatua matatizo
 * Mfundishe mtoto mipaka
 * Msaidie mtoto kujua hisia zake na za watu wengine

Usisahau kurudi tena kwaajili ya hatua nyingine za ukuaji wa mtoto!


SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania20/01/202124/07/2024Posted inUncategorizedLeave a
comment on 2. MALEZI YA MTOTO KATIKA UMRI WA UTOTO


MALEZI YA MTOTO NA UKUAJI WA MTOTO

Ukuaji wa mtoto

Hatua za ukuaji wa mtoto

Ukuaji wa mtoto umegawanyika katika hatua sita, kila hatua huleta uwezo na
matarajio mapya katika jamii na kutumika kama mapito muhimu katika ukuaji wa
mtoto

--------------------------------------------------------------------------------

1. Kabla ya kujifungua

Kabla ya kujifungua

Chembe moja kiumbe hubadilishwa na kuwa mtoto mwenye ajabu ya uwezo wa
kujibadilisha kwenda kwenye maisha katika mazingira ya duniani

Hatua kabla ya kujifungua

Kipindi cha kuota

Hiki ni kipindi kati ya utotoleshaji mpaka upandikizaji wa mtoto. Kipindi hiki
huchukua takribani siku 14

Kipindi cha kiinitete

Hiki ni kipindi kati ya upandikizaji mpaka kiinitete kimetengeza viungo vikuu
vya mtoo. Kipindi hiki huchukua takribani miezi 3. Katika kipindi hiki mtoto
viungo vyake muhimu hujitengeneza, huonyesha utofauti wa kijinsia na mtoto
huanza kujibu kichocheo cha moja kwa moja

Kipindi cha fetasi

Kipindi hiki kuanza mara tu mifupa ya mtoto inapoanza kuwa migumu. Huanza
takribani miezi 3 mpaka mtoto anapozaliwa

Kabla ya kujifungua kipindi cha kiinitete ni kipindi muhimu sana. Ukuaji wa
fetasi katika tumbo huwa wa haraka katika kipindi cha kiinitete. Hali isiyo ya
kawaida katika viungo vya mtoto inaweza tokea. Tuwe makini sana na kuzingatia
katika kipindi hiki ili kumlinda mtoto

Ukuaji wa akili ya mtoto

Ukuaji wa akili wa mtoto huanza ndani ya siku 30, ifikiapo siku ya 40 adi 100
saizi ya ubongo huongezeka. Ifikipo miezi mitano sehemu muhimu za akili ya mtoto
huanza kukua. Miezi tisa akili ya mtoto inakuwa tayari kwaajili ya mtoto kuweza
kuzaliwa

Maendeleo ya uwezo wa utambuzi

Wakati mtoto yupo tumboni huanza kujifunza lugha kutoka kwa mama ake. Mtoto
akiwa tumboni husikiliza mazungumzo ya mama ake katika wiki 10 za mwisho za
ujauzito na wakati wa kuzaliwa huenda akaonyesha alichokisikia

Maendeleo ya uwezo wa kihemko wa kijamii

(Afya ya mama mjamzito na mtoto)

Ulinzi wa mtoto huanza kwa kumlinda mama anayetarajia kujifungua mtoto. Utafiti
unaonyesha mama wajawazito wenye msongo wa mawazo na unyanyasaji wa kimwili
hujifungua watoto wachanga wenye kasoro

Mama mjamzito apate msaada wa familia. Uwepo wa mwenza mwenye huruma na watu
wengine wenye msaada katika familia,kazi chache za nyumbani na ajira dhabiti

Mama mjamzito hatakiwi kuwa na msongo wa mawazo, hupelekea mama mjamzito
kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo sana

Pombe kwa mama mjamzito ni hatari, mama mjamzito atumiapo pombe hupelekea
madhara kwa mtoto. Mtoto anaweza kupata kichwa kidogo kisichokuwa cha kawaida,
ukuaji mdogo wa akili ya mtoto,magonjwa ya moyo na matatizo ya viungo

Swali: Kwanini wanawake wanatoa mimba? Tufanye nini kuzuia utoaji wa mimba?


SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania20/01/202124/07/2024Posted inUncategorizedLeave a
comment on MALEZI YA MTOTO NA UKUAJI WA MTOTO


MALEZI MTOTO MAZURI

Malezi mazuri ya mtoto

Kumlea mtoto ni kazi moja wapo ngumu na ni ya lazima kuitimiza hapa duniani,
kazi ya malezi inaweza ikakufanya ujione pengine hukuwa tayari kumlea mtoto

Videkezo vinavyoweza kukusaidia katika malezi mazuri ya mtoto wako

Malezi ya mtoto sio rahisi, malezi ya mtoto ni kazi ngumu

1. Kukuza kujithamini kwa mtoto wako

Mtoto huanza kujithamini kwa kujiona wao wenyewe kupitia macho ya wazazi wao.
Sauti yako, lugha ya mwili wako na kila tendo huchukuliwa na mtoto. Matendo na
aneno yako kama mzazi huathiri kujithamini kuliko kitu kingine chochote. Tumsifu
mtoto anapoonyesha mafanikio ata wakifanya dogo na tuwafanye wajisikie fahari.
Tumruhusu afanye vitu mwenyewe hii itamsaidia ajione anauwezo wenye nguvu ndani
ake. Tusimlinganishe mtoto na mtoto mwingine atajiona hana thamani. Tusitumie
maneno makali kwa mtoto, tuchague maneno kwa umakini. Mjulishe mtoto wako kila
mtu hukosea na bado unampenda hata kama hupendi tabia yake

2. Kuwa mfano mzuri wa kuigwa na mtoto

Usimwambie mtoto unachotaka akifanye, muoneshe kwa vitendo unachotaka afanye.
Mtoto huangalia kwa umakini kila kitu mzazi anachokifanya. Mzazi kumlea mtoto
kwa vitendo itamsaidia zaidi kuliko maneno. Mfanye mtoto wako awe unavyotaka kwa
vitendo zaidi

3. Tafuta mda kwaajili ya wako

Imekuwa ngumu sana kwa wazazi na mtoto kupata mda wa kuwa pamoja. Mzazi ni
lazima utafute mda wa kuwa pamoja na mtoto ata kama umetingwa na kazi kiasi
gani, angalau dakika kumi kila siku, siku moja kwa wiki, wiki moja kwa mwezi na
hata likizo moja kwa mwaka kutokana na jinsi mazingira yalivyo kati yako na
mtoto. Mpe mtoto nafasi ya kuchagua jinsi gani mtatumia muda wenu

4. Yape mawasiliano kipaumbele kati yako na mtoto

Mzazi usimpe tu amri mtoto afanye nini, mtoto anataka maelezo na anastahili
maelezo kama watu wazima. Wazazi wanaompa mtoto nafasi katika maamuzi na kumpa
maelekezo humsuruhusu mtoto kuelewa na kujifunza kwa njia isiyo ya usimamizi.
Yaweke matarajio yako wazi kutoka kwa mtoto, kama kuna tatizo elezea, mruhusu
mtoto mtafute suluhisho kwa pamoja na mruhusu mtoto achague suluhisho linalofaa
zaidi kisha toa maoni yako

5. Mpende mtoto na muoneshe kwa vitendo

Hakuna kitu muhimu kama kumpenda mtoto wako kupita kiasi. Kumpenda mtoto kupita
kiasi si kumuharibu mtoto, mpende sana mwanao. Unachomoa mtoto au kumfanyia kwa
jina la upendo hapo ndipo tumemuharibu mtoto. Kumpenda mtoto inaweza kuwa rahisi
kama utamkumbatia, kutumia muda wako na yeye na kusikiliza maswala yao

6. Mpe mtoto malezi mazuri na thabiti

Mpe mtoto wako uzoefu mzuri, atakua na uwezo wa kuwa na uwezo mzuri yeye
mwenyewe na atawapatia na wengine. Uwezo mzuri humsaidia mtoto kiakili na
kutengeneza kumbukumbu zako ambazo ni fahari katika maisha ya mtoto wako. Kuwa
mzazi bora ni pamoja na kumfundishs mtoto wako mazuri na mabaya. Kuwa mpole
unapomuelekeza mtoto, zingatia sana jambo linalomfanya mtoto awe na tabia
alizonazo pia uifanye nafasi ya kujifunza kwaajili ya badae

7. Kuwa mahali salama kwa mtoto wako

Acha mtoto wako ajue kwamba siku zote utakukuepo pembeni yake kwa kuwa
muwajibikaji kwa ishara za mtoto na kuhisi mahitaji yake. Utamoa msaada na
kumkubali mtoto  wako. Msikilize mtoto kwa maendeleo Bora ya uthibiti wa mhemko

Kitu kizuri ni kwamba, japokuwa malezi ni magumu lakini yana zawadi yake. Sehemu
mbaya ni zawadi ya malezi huja baada ya kazi ngumu. Lakini kama tutajitahidi
Sasa tutavuna thawabu na hakuna kitu cha kujutia




SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania13/01/202124/07/2024Posted inUncategorizedLeave a
comment on MALEZI MTOTO MAZURI


MALEZI YA MTOTO

Wote tumekuwa tukitaka kuwa wazazi bora kwa watoto wetu lakini ushauri umekuwa
mwingi katika kuwakuza watoto ili wawe na uwezo wa kujiaamini, rafiki na mwenye
mafanikio. Ni muhimu sana kuweka uwiano katika vipaumbele, majukumu, mahitaji
muhimu ya mtoto wako, wanafamilia wengine na wewe mwenyewe. Hapa tutajadiliana
jinsi gani tunaweza kuwasaidia watoto wakue na kuwa, wewe kama mzazi unataka
bila kupotea wakati wa malezi ya watoto wetu.

Malezi ya watoto ni nini?

Malezi ya watoto ni hatua za kuwakuza watoto na kuwapatia ulinzi wa kutosha
unaoambatana na kujali ili kuhakikisha wanapokuwa watu wazima wawe waliokuwa
bora.

Malezi mazuri ya watoto ni yapi?

Malezi mazuri ya watoto ni yale yanayohusisha uthabiti, ratiba na kuwapatia
watoto hisia ya kudhibiti. Malezi mazuri ya watoto humpa mtoto uhuru katika
kukua na kuwalea watoto kwa kuzingatia umri wa mtoto na hatua ya ukuaji
aliyofikia.

Malezi mazuri ya watoto

Aina ya malezi ya watoto.

Kitu kimoja kinachotia hamasa kuwa mzazi ni utofauti jinsi tunavyokuza watoto
wetu. Na wakati huohuo kuna vitu vingi vimezoeleka kutoka kwa wazazi tofauti.
Watafiti wamejaribu kueka makundi manne ya malezi kutokana na jinsi wazazi
wanavyolea watoto wao.

1. Malezi ya kimabavu/ubabe

Malezi ya kibabe

Wazazi uwalea watoto wao katika misingi ya nidhamu, watoto hutakiwa kuwa na
nidhamu ya hali ya juu na akifanya kosa la utovu wa nidhamu ni lazma kuadhibiwa
vikali na wazazi. Mzazi ndiye kila kitu katika makuzi ya mtoto, hueka sheria na
nakutoa amri kwa mtoto bila kumpa nafasi na ata maelezo kwa watoto. Watoto
hulelewa katika mazingira ya ukali sana na kupangiwa kila kitu na wazazi. Hakuna
mawasiliano ya kutosha kati ya wazazi na watoto. Matarajio kutoka kwa watoto ni
makubwa lakini yasiyo kuwa uhuru. Mfano; Mtoto anaweza akawa na ndoto ya kuwa
mchoraji wazazi wakataka ni lazima awe rubani.

2. Malezi ya kudekeza

Malezi ya kudekeza

Wazazi uwalea watoto kwa kuwaacha wafanye wanachokitaka na kuwapatia muongozo
kidogo sanawa kile wanachokifanya. Wazai huwa marafiki zaidi kwa watoto kuliko
wazazi, husimamia nidhamu wastani na si kwa hali ya juu. Watoto hugundua na
kutatua matatizo yao wao wenyewe na pia mtoto huusishwa katika maamuzi na ata
kufanya maamuzi yao wenyewe na sio kutoka kwa wazazi. Mawasiliano huwa ni
makubwa kati ya mtoto na wazazi na mara nyingi yanaweza yakawa yakupitiliza.
Matarajio kutoka watoto ni madogo na mara nyingi anayajua mtoto mwenyewe. Mfano;
Watoto wa shule ya sekondari wasiopeleka ripoti zao za matokeo kwa wazazi ni wao
wenyewe ndo wanajua wanatarajia kupata matokeo ya aina gani katika mitihani yao
ya kumaliza elimu yao ya sekondari.

3. Malezi huru

Malezi huru

Wazazi huwapa watoto uhuru uliopitiliza, watoto hurura mitaani na wazazi hajui
ata watoto wako wapi. Wazazi hawajui watoto wao wamekula nini, wamevaa nini na
hata wapi wamelala. Wazazi hawana mda na malezi ya watoto na hata kujua wafanye
nini katika malezi ya watoto. Hakuna nidhamu katika aina hii ya malezi ya
watoto, watoto huachwa wafanye chochote wanachokitaka bila muongozo wowote.
Hakua mawasiliano kati ya wazazi na watoto na kama yapo ni madogo sana.
Matarajio kutoka kwa watoto ni machache sana au yasiwepo kabisa. Mfano; Watoto
wanaweza wakawa hawafiki shuleni lakini wazazi wakawa hawana taarifa kwa sababu
hawatengi muda wa kwenda kufuatilia maendeleo ya mtoto shuleni.

4. Malezi ya muafaka

Malezi muafaka

Wazazi huwa na busara, walezi na hupanga matokeo ya hali ya juu na matarajio
kutoka kwa watoto. Watoto huwa na nidhamu na kujitunza wenyewe. Sheria za
nidhamu huelezewa kwa sababu gani zimewekwa. Aina hii ya malezi ndio inafaa
zaidi kwa watoto. Mazungumzo ni mara kwa mara na yanayoendana na umri/uelewa wa
watoto. Matarajio kutoka kwa watoto ni makubwa lakini yanayotambulika. Watoto
wanaweza kuwa sababu ya matarajio yao.

Je ni aina gani ya malezi ya watoto ninayotumia?

Wachache wetu hutumia aina moja ya malezi ya watoto, lakini ni vizuri kuwalea
watoto kwa aina mbalimbali za malezi ya watoto. Mfano; Wazazi anaweza asitumie
malezi ya ubavu, lakini nyakati katika malezi ya watoto inahitajika atumie aina
hiyo ya malezi ya watoto.

Wakati ni rahisi kumlea mtoto pale wazazi wanapotumia aina moja ya malezi,
baadhi ya utafiti unaonyesha kama mzazi mmoja akitumia malezi ya kimabavu
itamsaidia mtoto zaidi kuliko wote watumie malezi ya kudekeza.

Kama umefurahishwa na chapisho hili, tafadhali sambaza kwa ndugu, jamaa na
marafiki!


SHARE THIS:

 * Twitter
 * Facebook
 * 

Like Loading...
Posted byparentingTanzania06/01/202103/07/2024Posted inParenting2 Comments on
MALEZI YA MTOTO
 * Home
 * About
 * Blog
 * Contact

parentingTanzania, Blog at WordPress.com.

 * Subscribe Subscribed
    * parentingTanzania
      
      Sign me up
    * Already have a WordPress.com account? Log in now.

 *  * parentingTanzania
    * Customize
    * Subscribe Subscribed
    * Sign up
    * Log in
    * Report this content
    * View site in Reader
    * Manage subscriptions
    * Collapse this bar

 

Loading Comments...

 

Write a Comment...
Email (Required) Name (Required) Website

Privacy & Cookies: This site uses cookies. By continuing to use this website,
you agree to their use.
To find out more, including how to control cookies, see here: Cookie Policy
%d
Design a site like this with WordPress.com
Get started